

Nimekuwa kama makaa.
Uzuri wangu umechomeka
Nimebakia Ganda la ndizi.
Nawaumiza wanaonihimiza pia.
Sikupenda kuwa hapa,ni Hali Tu.
Usingizi natamani sipati
Ya kale niliyojivunia sijuti
Nimebakia kama sanamu ardhini
Nimekosa sana Amani
Sikupenda kuwa hapa,ni Hali Tu.
Japo Kula nakula,sishibi
Huku nje natembea,watu siwaoni
Salamu zao hazinifikii,masikio nimeifunga
Kofia yangu naivaa,macho nazikinga
Sikupenda kuwa hapa,ni Hali tu.
Mapenzi yangu ya soka haipo tena
Utamu wake siujui tena omena.
Aisha naye anajaribu sana asinipate
Mamangu amenitafutia daktari Hadi pate
Sikupenda kuwa hapa,ni Hali Tu.
Najua fikra hazitoisha kichwani
Na Hali haitorejea zamani
Naiona chakula hii mezani
Nafahamu utamu wake lakini sikitamani
Sikupenda kuwa hapa,ni Hali Tu.
Nataka Amani yangu,
Natamani niketi nafasi zangu,
Nitarejesha furaha yangu,
Lakini bado sina ujuzi wa kuindoa huu uchungu
Siipendi Hali hii,nasikitika.