

Miaka na mikaka
Ulimwengu nmetembea
Viatu vyaweza nena
Milima na mabonde nimepitia
Miaka na mikaka
Nyumbani kutamu
Utamu wa kukaa bure
Ila chakula hakuna
Mikono tumenawa
Mara mia kwa siku
Ila tumboni hakuna
Kunawa mikono bila lishe Kuna haja gani?
Kila siku nitembeapo
Kartasi za kazi nimebeba mfukoni
Barua za kuomba kazi nimeandika na kutuma ofisi mbalimbali
Lakini hakuna jibu kamwe
Kazi nimetafuta kwa miaka mingi
Ili watoto wapate karo,chakula na malazi
Mahitaji nyumbani chungu nzima
Kazi hakuna, chakula hakuna
Ndugu zangu wanitegemea
Ndiposa niwatimizie mahitaji yao
Kilio cha huzuni
Kimekunja nyuso zao
Fikra zimeniadama
Miba ya umaskini imedunga maisha yetu
Machozi ya damu yametiririka hadi moyoni
Kazi hakuna,pesa hakuna, nyumbani hakuna chakula …ni kilio tu ,,jameni tufanyeje??
@Januaris Musyoka