

Kitandani amelala kwa miaka
Hakuna wa kumjali
Hakuna wa kumkumbuka
Je alikosea wana wake?
Wana wake ndio wamemtega?
Ni kosa gani mzee katenda?
Ugonjwa unamuumiza hospitalini
Fikra zinamuumiza akili
Amewasomesha wana wake
Lakini hakuna anayemjali
Bar hawatoki
Kulipwa wanalipwa lakini kazi ni kulewa tu
Nani atamnusuru huyu mzee
Amekula chumvi nyingi
Ugonjwa unamuumiza kitandani
Je ni maadili ama utu wana wake wamekosa?
Shamba wameliuza
Pesa zote kwa mama pima
Maskini mzee anaumia
Huzuni moyoni mwake
Unakatakata moyo wake
Nani atamnusuru maskini mzee apate matibabu
@januaris