

Mwanangu ipo siku,
Maulana katupangia,
Siku zinakuja,
Za furaha na za kusherehekea,
Siku zenyewe zikifika,
Shamba tutamiliki,
Kulima tutalima, kujenga tutajenga,
Kazi tutazifanya,
Bila ubanguzi wa jinsia,
Hata kama baba yako alitufurusha,
Kuishi tutaishi,
Kwani Mola yunasi,
Anatulinda,
Hata tukibanguliwa,
Jinsia ya kike kaonewa,
Tufanye juu chini,
Kutetea haki zetu wanawake,
@Januaris