Ni Haki

Maji unayavulia nguo,

Ili upate kuondoa uchafu mwilini

Nguo ulizozifua,

Enda kazivae.

Ulivyopaka kichwa sabuni,

Ndivyo unavyonyolewa.

Vivyo ndivyo ilivyo,

Kijijini tunamoishi.

Kunazo desturi na mila,

Zinazokandamiza akina mama.

Vile vile kunazozinawapa kipaumbele,

Na kuwapa haki zao wanawake.

Kazi wanafaa kupewa,

Wafanye bila ubanguzi.

Wengi wao wameajiriwa,

Na kuendeleza maendeleo ya jamii ilivyo.

Familia wamezilea,

Na kuongoza katika vikundi.

Tuwape wanawake kipaumbele,

Na tuwache kuwabangua.

Katika uongozi wa nchi,

Wameweza kuonyesha ujasiri katika uongozi.

Tuwape heshima na wakati,

Ili wafanye kazi iwezekanavyo.

Tuwache porojo na kuwaongelelea vimbaya.

Sote tukiwapa wanawake kipaumbele,

Jinsia ya kike itanawiri na kuleta maendeleo nchini.

@Januaris Musyoka

About the Author

Leave a Reply

You may also like these

No Related Post

error: Content is protected !!

Discover more from Osprey Empire

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading