NIRUSHIE KAKITU- CHALLENGE

Hello sijui kama unaniskia
Mimi ni ule niece mpole kutoka Tanzania
Nimebania kwenye inbox kuingia
Nikueze yaliyonifikia
Nilisema kuiba sitothubutu
But usiponirushia kakitu
Nitakosa utu
Nibebe silaha butu
Naishi kwa utatanishi
Na kwa aushi sibishi
Ila kwa jirani sibishi
Hata kama hawatishi
Nirushie kakitu
Juu hata chakula nimekosa
Na mtondo naenda kuposa
Pia sina mahari
Ila nirushie kwa hiari
Nafikiri maisha ya kifahari
Kwenye bahari bila habari
Natafakari ya babu
Aliniambia nisiwe na aibu
Kama sina nisiwe zuzu au bubu
So nisaidie mjomba
Angalau nisome nijenge nyumba
Fanya kweli usikose la kuamba
Nirushie kakitu naomba

MayakaPoetry

ThePassionatePursuitOfPoetry

About the Author

Leave a Reply

You may also like these

error: Content is protected !!

Discover more from Osprey Empire

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading