

Nimeubeba wangu gunia
Nishachoka na za dunia
Kamwe sitakuvumilia
Kisirani za kushoto kulia
Nimechoka kujishikilia
Penzi lako limekuwa bandia.
Jumapili tulifunga ndoa
Kwa wazazi ukaniondoa
Penzi ushalitia madoadoa
Ibada gani itakuokoa
Ona Sasa nakohoa
Duniani hili gonjwa taniondoa.
Juzi juzi ulioa Maria
Kesho yake ukaleta Sofia
Mpenzi wangu nilikulilia
Naye baba kakupa wosia
Kupata gonjwa hukuhofia
Kwa jua hukutumia kofia.
Ulienda kazi baharini
Ukabobea usheratini
Sifa ulieneza kilabuni
Hukununua hata sabuni
Nyumbani ulitaka maini
Hata senti haikuwa mfukoni.
Moyoni umenibondabonda
Ukaniambukiza kaswende
Ubinadamu ulifungia ndi!
Dhuluma imepata kishindo
Mwakani naumwa mkundu
Mpenzi nalia aaa..!!!
Ndoa kweli baraka
Kwangu mimi kiraka
Nilikuzalia kina Kalaka
Lakini sasa nipe talaka
Ndoa hii niliitaka
Hivi sasa ni takataka.