

Adui mpende ila usimtende. Yule umdhaniaye ndiye rafiki huenda akawa mnafiki. Akose kukufaa hata siku ya dhiki.
Dunia ni mviringo Kuna wale wanyenyekevu na wenye maringo. Yaruhusu majira magumu. Kukuashiria wale wa kudumu.
Yule rafiki wa maishani Huenda akakuacha ukiwa mashakani. Na asijawe na huruma tumaini lako likipukutika kama majani
Wakati mwingine familia zimegeukana. Pasiwe na yeyote aliye na ari ya kusaidiana. Mara ngapi tumeskia baba kampokonya mwanawe mchumba? Tamaa ishamfanya kumkosea heshima muumba.
Wengine wetu machozi tumepanguzwa na tusiowajua. Chakula tukalishwa na tusiowatambua. Na wakati mwingine tumaini la kupona tukapewa na wanaougua. Kwani wewe hujaskia kikulacho ki nguoni mwako?
No Related Post