

Bona dhuluma?
Nauliza bona dhuluma?
Kijana yatima anaonewa huyu
Hawezi tembea Tena
Jirani yake kamkata miguu yake
Sasa hawezi tembea wala kukimbia
Shida zinamuandama
Hawezi fanya kazi ila za ofisi
Kazi zenyewe ni nadra sana
Tena lazma utoe kitu kidogo
Uso wake umekunjana
Mikono yake ameinyoosha kuomba usaidizi siku mzima
Sasa anatembea na wheelchair
Mawazo yamemkula akili
Nani atasomesha watoto wake?
Nani anamnusuru kupata haki?
Bona jirani yake kamdhulumu?
Anajuta kwanini alizaliwa kuteseka
Maumivu ya miguu yanamuumiza
Jirani yake anataka kumuagamiza
Sababu za mipaka ya shamba
Je suluhisho ni gani?
@Januaris